1 Oktoba 2024 - 11:01
Kuanza rasmi kwa mashambulizi ya ardhini ya jeshi la Kizayuni katika ardhi ya Lebanon

Jeshi la Kizayuni limetangaza kuanza kwa operesheni zake za ardhini nchini Lebanon.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Jeshi la Kizayuni limetoa taarifa na kutangaza kuanza kwa operesheni zake za ardhini nchini Lebanon.

Kwa mujibu wa taarifa hii, operesheni za ardhini za jeshi la Kizayuni zitakuwa za kiuzingativu zaidi zikisapotiwa na vifaru na mashambulizi ya anga ya ndege za kivita kusini mwa Lebanon.

Msemaji huyo wa jeshi la utawala wa Kizayuni amesema kuhusiana na hilo kwamba: Vikosi vya jeshi la Israel vimeanza operesheni ya ardhini iliyokusudiwa na kubainishwa dhidi ya maeneo yanayolengwa na Hezbollah katika eneo la karibu na mpaka wa Kusini mwa Lebanon.